Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajadili mustakhbali baada ya 2015 Msumbiji

Ban ajadili mustakhbali baada ya 2015 Msumbiji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko ziarani nchini Msumbiji ambako Jumatatu amekutana na spika wa bunge la nchi hiyo Bi Veronica Makamo na kushiriki mjadala wa “ Mustakhbali tunaoutaka baada ya malengo ya milenia 2015 na ajenda za 2025”.Katika mjadala huo Ban amesisitiza kwamba mustakhbali ambao dunia inautaka ni mtazamo wa kimataifa na njia ya kuelekea huko ni ndefu na ngumu. Amesema ili kufanikisha azima hiyo viongozi kila mahali wanatakiwa kujitoa kimasomaso.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)