Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea wasiwasi kutokana jaribio la Kombora lililofanywa na Korea Kaskazini

Ban aelezea wasiwasi kutokana jaribio la Kombora lililofanywa na Korea Kaskazini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ameingiwa na hali ya wasiasi kufuatua mvutano baina ya Korea mbili, ambazo zimeingia kwenye msuguano uliosababishwa na kitendo cha Korea ya Kaskazini kurusha kombora la masafa ya katika bahari.

 

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Korea imekuja huku kukiwa na mashinikizo makali toka jumuiya ya kimataifa ikiwemo Ban  mwenyewe ambaye aliitaka Pyongyang kutoanzisha hali yoyote inayoweza kusababisha kuongezeka kwa mivutano.

 

Jaribio hilo limetoa msukumo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza mbinyo wa vikwazo ambapo sasa mbinyo huo umeongezeka hadi kwenye maeneo ya kibiashara na shughuli za kibenki.Kwa upande mwingine, Ban amesema kuwa yuko tayari kufanikisha majadiliano ya pande hizo mbili ili kuondosha mikwaruzano.