Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UPU yaendelea kusaidia umarishaji wa huduma za posta Palestina

UPU yaendelea kusaidia umarishaji wa huduma za posta Palestina

Umoja wa mashirika ya posta duniani, UPU umerejelea azma yake ya kutoa msaada wa kiufundi ili kuboresha huduma za posta huko Palestina.Assumpta massoi na taarifa zaidi

(RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa UPU Bishar Hussein huko Berne Uswisi baada ya mazungumzo yake na Waziri wa Mawasiliano wa Palestina SafarNasserEldin ambapo UPU italipatia shirika la posta la Palestina zaidi ya dola Laki Moja.

Fedha hizo zitatumika kununua vifaa muhimu vinavyohitajika kamavile magari ya kusafirishia vifurushi na barua, jenereta za umeme na vifaa vya kisasa vya kusomea  alama inayokuwa na taarifa kuhusu bidhaa au “barcodes”.

Bwana Bishar amesema hatua hiyo itawezesha shirika la posta Palestina kuboresha huduma zake kwa wateja na wakati huo huo kuongeza kipato na kuondokana na utegemezi kwa wahisani.