Haile Menkerios atakuwa Mkuu wa Ofisi ya UM kwenye AU: Ban

17 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Bwana Haile Menkerios wa Afrika Kusini kuwa mwakilishi wake maalum kwa Muungano wa nchi za Afrika, AU, na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kwenye AU. Bwana Menkerios pia ataendelea kushikilia wadhafa wake kama Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Sudan na Sudan Kusini.

Menkerios anairithi nafasi ya Zachary Muburi-Muita, ambaye muhula wake wa kuhudumu unahitmishwa mnamo Juni 30 mwaka 2013.

Bwana Menkerios ana uzoefu mkubwa kuhusu masuala ya bara la Afrika, kwani amewahi kuhudumu kama Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na pia kama Naibu Katibu Mkuu kuhusu Masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa, mwaka 2007- 2010

Bwana Ban amemshurukuru Bwana Muburi-Muita kwa huduma yake katika ofisi ya Umoja wa Mataifa kwenye Muungano wa Afrika, na kwa kuongeza ushirikiano baina ya bara la Afrika na Umoja wa Mataifa.