Rais wa Nigeria atangaza hali ya hatari katika majimbo ya Mashariki

17 Mei 2013

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari katika majimbo matatu yaliyoko Mashariki mwa nchi hiyo kufuatia uasi unaendeshwa na kundi la Boko Haramu ambao wanahatirisha mustakabala wa taifa.

Tayari kamishna ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali matukio ya mashambulizi yanayoendeshwa na kundi hilo ambalo linatajwa kuwa na mafungaano pia na mitandao mingine ya kigaidi nje ya nchi hiyo.

Ofisi ya Haki za binadamu imeitolea mwito serikali ya Nigeria kuchukua hatua sahihi kurejesha hali ya usalama pasipo kuziendea kinyume haki za binadamu.

Rais Jonathan amesema kuwa vitendo vya kufuruta ada vinavyoendeshw ana wanamgambo wa kundi hilo vinavuruga umoja wa kitaifa na kuliweka katika hali tete taifa kwa ujumla.