Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tokomeza ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja: Pillay

Tokomeza ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja: Pillay

Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsi zao, Umoja wa Mataifa umetaka nchi wanachama kuchukua hatua zaidi kutokomeza vitendo vya kikatili na ghasia dhidi ya makundi hayo. Ripoti ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA JASON)

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa masuala ya usagaji  na ushoga si mwiko tena kwenye Umoja wa Mataifa. Pillay anasema kuwa dhuluma zinazoendeshwa dhidi ya mashoga na wasagaji zinaendelea kwa viwango vya juu kila pembe ya dunia maana kwamba mengi yanahitajika kufanywa kuafikia ulimwengu ambapo kila mmoja yuko huru na anaheshimiwa. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa.

 (SAUTI YA RUPERT COLVILLE)