Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waahidi kuipiga jeki Tanzania kuboresha lishe bora

UM waahidi kuipiga jeki Tanzania kuboresha lishe bora

Umoja wa Mataifa umeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania kukabiliana na tatizo la lishe bora hasa wakati huu ambapo dunia inapiga mwendo kuelekea kwenye malengo ya maendeleo ya mellenia. George Njogopa na taarifa zaidi.(TAARIFA YA GEORGE)

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kitaifa yenye lengo la kuboresha hali ya lishe Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Bwana Paul Edward alisema kuwa, Tanzania imeendelea kupiga hatua kukabiliana matatizo yanayotokana na ukosefu wa lishe, lakini hata hivyo bado kuna safari ndefu.

Kumekuwa na idadi kubwa ya vifo vya kina mama wanaojiandaa kujifungua na vile vya watoto waliochini ya umri wa miaka hiyo mitano kutokana na kile kinachoelezwa kwamba ni ukosefu wa lishe bora.

Rais Jakaya Kikweye aliyezindua kampeni hiyo amesema kuwa serikali yake imedhamiria kukabiliana na tatizo hilo la lishe bora kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

Kampeni hii pia imelenga kupunguza kiwango cha watoto wanaandamwa na matatizo ya kudumaa ambao wanafiia asilimia 40 kwa sasa.