Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

"Nitakuza maendeleo ya dunia kwa biashara"- Dk Kituyi

"Nitakuza maendeleo ya dunia kwa biashara"- Dk Kituyi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Mukhisa Kituyi wa Kenya kuwa Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia Septemba mosi mwaka huu. Katibu Mkuu wa sasa Supachai Panitchpakdi anamaliza kipindi chake mwezi Agosti mwaka huu.Kufuatia uteuzi huo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya amefanya mahojiano na Bwana Kituyi ili kufahamu ana mtizamo gani katika nafasi hiyo ambapo anaanza kelezea namna alivyopokea uteuzi huo.