Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asema anafahamu hali ilivyo nchini Nigeria

Ban asema anafahamu hali ilivyo nchini Nigeria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon anasema kuwa anafahamu kuhusu hatua ya serikali ya Nigeria ya kutangaza hali ya hatari kwenye majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.Ban anasema kuwa anaelewa kuhusu ghasia na kuzorota kwa usalama  eneohilo.

Ban ametoa wito kwa makundi ya wanamgambo kusitisha mashambulizi yao akiongeza kuwa hakuna suluhu inaloweza   kupatikana kwa njia ya ghasia. Amewataka wahusika wote kuheshimu haki za binadamu  na kulinda maisha ya watu wa Nigeria.