Jesús Vázquez awatembelea wakimbizi wa Syria nchini Jordan

16 Mei 2013

Balozi mwema wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ambaye pia ni mtangazi maarufu wa runinga nchini uhispania Jesús Vázquez wiki ameitembelea Jordan kuangazia hali ya maelfu ya wakimbizi nchini Syria hususan watoto na kusaidia kuchangisha fedha zinazohitajika na UNHCR nchini Syria.

Akiwa kwenye kambi ya Za’atri balozi huyo amesema kuwa ziara yake ina lengo la kuwasikilika wale wanaotaabika na kusaidia kuchangisha fedha nchini mwake kukidhi mahitaji yao. Wakati wa ziara hiyo ya siku mbili nchini Jordan Vázquez pia alitembelea mji mkuu wa Amman ambapo alikutana na wakimbizi wa mijini na kujulishwa kuhusu matatizo wanayopitia. Akiwa kwenye kambi ya Za’atri ambayo inazidi kupanuka balozi huyo alikutana na wakimbizi na watoa huduma za misaada. Tangu mzozo kuanza nchini Syria machi mwaka 2011 zaidi ya watu milioni 1.4 wameikimbia Syria huku Jordan ikipokea wakimbizi 460,000.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter