Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mambo manane muhimu ya kufahamu kuhusu njaa nchini Mali:WFP

Mambo manane muhimu ya kufahamu kuhusu njaa nchini Mali:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema mwaka mmoja wa machafuko nchini Mali umeleta njaa kwa maelfu na maelfu ya watu. Ukame na umasikini uliokithiri pia vimesababisha athari kubwa.

Kwa mujibu wa WFP kuna mambo manane muhimu ya kuyafahamu kuhusu tatizo la njaa Mali na nini kinachofanywa na WFP kupeleka msaada wa chakula kwa mamilioni ya watu nchini humo.

Shirika hilo linasema moja ni kwamba hali ya usalama wa chakula na lishe Kaskazini mwaMali imezorota saana kufuatia mapigano Kaskazini yaliyowafungisha virago  watu 475,0000 na kuwa vigumu kuwafikia waliosalia.

Lakini pili kila familia moja kati ya tano nchini humo zinakabiliwa na njaa kali hasa maeneo ya Gao,Timbuktu na Kidal. Tatu takriban asilimia 15 ya watoto nchini Mali wanaugua utapia mlo uliokithiri, huku zaidi ya 1/5 ya watoto wanaotakiwa kuwa shule hawasomi wengi wao wakiwa ni wasichana.

Nne asilimia 49 ya watu wa Mali wanaishi chini umasikini uliokithiri huku UNDP ikiliweka taifa hilo namba 175 kati ya nchi 187  ikiwa na maendeleo duni. Tano WFP inatarajia kuwasaidia watu wapatao milioni moja nchini humo kwa mwaka huu pekee.

Sita MWFP inapeleka chakula Kaskazini mwa Mali kwa kutumia mpakani mwa Mali naNiger.Saba mbali na msaada wa chakula kwa wakimbizi wa ndani WFP pia inatoa msaada wa fedha taslimu ambazo zinatumika kununulia mahitaji.

Na mwisho mabalozi wa WFP Amadou na Mariam wote wanatokaMalina walikuwa mabalozi wema wa WFP mwaka 2010.