Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa ngono wakabiliwa DRC

Ukatili wa ngono wakabiliwa DRC

Ripoti ya pamoja ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, DRC, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia hususani ni ubakaji nchini humo, inaonyesha kwamba takribani wanawake 200 wamebakwa  katika kipindi cha mwezi November pekee mwaka jana.

Taarifa hiyo inaonyesha kwamba vitendo vya ubakaji vimekithiri zaidi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini ambako bado kuna vuguvugu la machafuko inakuja wakati hu ambapo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa  nchini humo MONUSCO umetoa mafunzo kwa maafisa polisi wa mahakamani ili kudhibiti vitendo vya ukatili wa kingono ambapo utekelezaji wa mpango huo utasimamiwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Msemaji wa shirika hilo Jumbe Omari Jumbe Amefanya na mahojiano na mwandishi wetu Joseph Msami juu ya usimamizi wa mpango huo na hapa anaanza kueleza naman IOM kwa kudhaminiwa na MONUSCO inavyotoa mafunzo kwa makundi muhimu nchini DRC .