Tusifumbie macho hasara za kiuchumi zitokanazo na majanga: Ban

15 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika uzinduzi wa ripoti ya tatu ya udhibiti wa majanga na kueleza kuwa hasara zitokanazo na majanga hazitaweza kudhibitiwa iwapo mikakati ya kupunguza athari za majanga haitapatiwa kipaumbele. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA ALICE)

Hotuba ya Katibu Mkuu Ban imesema wakati wa kufumbia macho mikakati ya kudhibiti majanga umepita na hivyo kila mtu anapaswa kuchukua hadhari dhidi ya majanga Amesema tathmini ya hasara zitokanazo na majanga katika nchi 56 inaonyesha kuwa hasara kutokana na mafuriko, matetemeko ya ardhi na ukame iliwekwa kiwango cha chini kwa asilimia 50, wakati hasara halisi ya moja kwa moja kwa karne ya 21 ni karibu dola Trilioni Mbili na Nusu.

 Amesema hiyo haikubaliki wakati nchi zina ufahamu wa kupunguza hasara na badala yake kupata faida kwa udhibiti huo.

(SAUTI YA BAN)