Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa WTO

Ban apongeza uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa WTO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekaribisha uteuzi wa Balozi Roberto Carvalho de Azevêdo kutoka Brazil kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la biashara duniani WTO. Taarifa imemkariri Bwana Ban akisema kuwa akiwa ashahudumuakamamwakilishi kwenye shirika la WTO Balozi Carvalho de Azevêdo yuko kwenye nafasi nzuri  ya kuhakikisha kuwa WTO imeendelea na majukumu yake  muhimu kuhakikisha kuwa bishara inendelea bila kuwepo ubaguzi. Amesema kuidhinishwa kwa Balozi Azevedo na baraza kuu la WTO ni muhimu na umekuja wakati muafaka. Katibu Mkuu Ban amesema yuko tayari kushirikiana naye kuhakikisha kuwa biashara ya kimataifa imeafikia ukuaji kuweza kukabiliana na umaskini na kuwepo kwa maendeleo ya kudumu duniani.