Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO mbioni kuanzisha machapisho kwa digitali

UNESCO mbioni kuanzisha machapisho kwa digitali

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO  limepanga kutoa machapisho yake kwa njia ya digitali hatua ambayo itawawezesha mamilioni ya watu duniani kote kupata fursa ya kufikiwa na taarifa hizo bila malipo yoyote.Hatua hii inafuatia makubaliano yaliyofikiwa na bodi ya wakurugenzi ya shirika hiyo na hivyo kuwa ni taasisi ya kwanza ndani ya Umoja wa Mataifa kuanzisha sera inayotoa fursa kwa taarifa zake kupatikana kirahisi.

Sera hiyo mpya ya kuanzisha machapisho kwa njia ya digitali ilitangazwa na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Janis Karklins,wakati wa kongamano la kimataifa linalofanyika Geneva, uswis likiwa ni kongamano la mawasiliano na habari.