Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR Burundi imefungua kambi mpya ya wakimbizi wa Congo:UNHCR

UNHCR Burundi imefungua kambi mpya ya wakimbizi wa Congo:UNHCR

Nchini Burundi, wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambao wanakimbilia usalama wao kutoka mashariki mwa nchi hiyo, watawekwa kwenye kambi mpya ya Kavumu katika mkoa wa Cankuzo.Kambi hiyo ambayo itafunguliwa hapo kesho Jumatano, Mei 15 na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Ina uwezo wa kuhifadhi hadi wakimbizi 13,000, na inatarajiwa kuwa makazi ya wakimbizi 5,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2013.  Ramadhani Kibuga anaarifu toka Burundi

 (RIPOTI YA RAMADHAN KIBUGA)