Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya kilimo ni fursa ya ajira:ILO/UNCTAD

Biashara ya kilimo ni fursa ya ajira:ILO/UNCTAD

Kitabu kipya kilichohaririwa na shirika la kazi duniani ILO na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uchumi na biashara UNCTAD kinasisitiza kwamba biashara ya kilimo inaweza kuwa fursa nzuri ya kuunda nafasi za ajira  na kutokomeza umasikini duniani.Kitabu hicho chenye kichwa “kugawana mavuno:kilimo, biashara na ajira”kimetolewa leo.

Kitabu hicho ambacho ni matokeo ya utafiti wa UNCTAD na ILO uliodhaminiwa na Muungano wa Ulaya unasema kwamba sera muhimu zitoe kipaumbele katika kilimo.

Matokeo ya utafiti huo uliokusanywa katika miradi mbalimbali yanaonyesha uhusiano mkubwa baina ya kupunguza umasikini kwa upande mmoja na umuhimu wa kiloimo na biashara katika upande mwingine.

Pia umesisitiza kwamba  kilimo kina jukumu kubwa katika kuinua uchumi hasautoaji wa nafasi za ajira.

Kwa mujibu wa ILO kilimo kinaajiri watu zaidi ya bilioni moja katika nchi zinazoendelea ambazo zinawasilisha asilimia 48 ya ajira duniani.

Kitabu kimejumuisha uchunguzi wa miradi ya kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu athari za ajira katika biashara ya kilimo. Kimependekeza kuwalinda wafanyakazi wa sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji ili kwenda sambamba na ushindani katika masoko ya kimataifa.