Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulizi la Benghazi

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulizi la Benghazi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulizi la bomu ambalo lilipigwa katika mji wa Benghazi nchini Libya ambalo lilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.Baraza hilo limesema kuwa limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la shambulizo hilo lililofanyika May 13 na limewapa pole waathirika na serikali kwa ujumla.

Limetaka wahusika wa tukio hilo kusakwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria huku likisisitiza kutofumbia macho vitendo vyovyote vya kigaidi.