Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tufani Mahasen kuikumba Myanmar na Bangladesh

Tufani Mahasen kuikumba Myanmar na Bangladesh

Nchini Bangalesh na Myanmar mapema leo wametangaza tahadhari na mikakati ya kukabiliana na tufani Mahasen inayotarajiwa kukumba maeneo hayo muda si mrefu. Mashirika ya Umoja wa Mataifa hususani lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yamesema yako tayari kuzisaidia nchi hizo  ambapo linasema linatiwa hofu na hali ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la Rakhine. Wakimbizi takribani 69,000 wako katika hatihati ya kuhamishwa na shughuli hiyo imeanza katika maeneo matatu. Kwa upande wake shirika la kuhudumia watoto UNICEF linasema linapeleka wafanyakazi wake , madawa na watakuwa tayari kufanya tathimini huku uongozi wa Rakhine ukiwa umetenga maeneo maalumu kwa ajili ya wakimbizi wa ndani na jamii zinazoishi pwani. Umoja wa Mataifa unasema maandalizi yote ya muhimu yanahitajika ikiwa ni pamoja na chakula cha dharura ambapo WFP inasema imeshatoa kitakachotosheleza kwa mwezi mzima wa Mei kwa wakimbizi wa ndani karibu 125,000 katika jimbohilo. Pia limeweka tayari tani zingine 4000 za mchele zitakazotosheleza kulisha watu 296,000 kwa mwezi mmoja.