Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DRC kutoka Angola wasaka huduma za kibinadamu: IOM

Wakimbizi wa DRC kutoka Angola wasaka huduma za kibinadamu: IOM

Takribani wakimbizi Elfu  40 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wanaorejea nyumbani kutokaAngolawametindikiwa na huduma za kibinadamu katika eneo liitwalo Kamako mpakani mwa nchi mbili hizo. Wakimbizi hao wanarejea nyumbani kufuatia ilani ya serikali yaAngolaya kuwataka wawe wamerejea makwao ifikapo kesho tarehe 15 mwezi huu.  Wakimbizi hao waliofurika katika eneo hilo wanalazimika kukimbilia mashuleni na kwenye makanisa ili kupata malazi wakati huu ambapo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, likihaha kuwanusuru. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)