Sheria dhidi ya mashirika yasiyo ya kibiashara Urusi ni kandamizi: wataalamu huru UM

14 Mei 2013

Wataalamu huru watatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za bindamu wameeleza wasiwasi wao mkubwa juu ya mazingira ya kihasama ambayo mashirika yasiyo ya kibiashara nchini Urusi yanakumbana nayo kutokana na sheria mpya iliyopitishwa mwezi Novemba mwaka jana.  Wataalamu hao kuhusu uhuru wa kujumuika, utetezi wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza wametaka sheria hiyo iangaliwe upya kwa kuwa inakinzana na sheria za kimataifa na ina madhara kwa mashirika yasiyo ya kibiashara ambayo yanafanya kazi kulinda haki za binadamu.  Mathalani wamesema mashirika yanayotetea haki za kisiasa na ambayo yanapata ufadhili wa kigeni yanaweza kuonekanakamamamluki iwapo yatadhindwa kukidhi vigezo vya sheria hiyo. Mmoja wao Maina Kiai ambaye anahusika na haki ya kujumuika amesema hofuyaojuu ya sheria hiyo mpya imepatiwa uthibitisho kwa kuwa hivi sasa wanashuhudia upekuzi dhidi usio wa kawaida dhidi ya mashirika hayo na hata mengine yamefunguliwa kesi na kutozwa faini kubwa.  Naye Margaret Sekaggya amesema wameshaonya kuwa masharti magumu ndani ya sheria hiyo kwa mashirika yanayohusika na haki za kisiasa yanaweza kukandamizi haki za watetezi wa haki za binadamu kuibua masuala  ya haki za binadamu na kufanya kaziyaoya utetezi.