Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vipya vya virusi vya Corona vyabainika Saudia

Visa vipya vya virusi vya Corona vyabainika Saudia

Wizara ya afya ya Saudi Arabia leo Jumanne imetangaza kusajiliwa kwa visa vingine vipya vinne vya virusi vya Corona  kwenye jimbo la Mashariki mwa nchi hiyovinavyosababisha matatizo ya kupumua. Wizara hiyo inasema mgonjwa mmoja aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na wengine watatu bado wako hospitali. Shirika la afya duniani WHO linasema limekuwa likitathimini idadi ya vifo vilivosababishwa na virusi hivyo ambapo hadi sasa ni kati ya 18 na 20 duniani kote, na visa vyote kwa jumla vilivyothibitishwa maabara vimefikia 38.