Gesi ya cabon angani imeongezeka sana:UNFCCC

13 Mei 2013

Amesema kuwa viwango vya sasa vya gesi ya Carbon vya mianne kwa milioni ni vya kihistoria  na sasa ulimwengu umeingia wakati wa hatari. Amesema kuwa ulimwengu ni lazima ugutuke na kuchukua hatua kwa usalama wa mwanadamu  na mandeleo ya kiuchumi.

Amesema kuwa kinachohitajika ni kuwekwa sera ambazo zitakabiliana na hali iliyo sasa. Ameongeza kusema kuwa bado kuna fursa ya kuondoa athari za mabadiliko ya hali ya hewa kupitia kwa pande tatu kuu  zikiwemo jamii ya  kimataifa, serikali na sekta za biashara na fedha.