Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha hukumu dhidi ya kiongozi wa zamani Guatemala

Pillay akaribisha hukumu dhidi ya kiongozi wa zamani Guatemala

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha hukumu ya kwanza kabisa dhidi ya kiongozi wa zamani nchini Guatemala José Efraín Ríos Montt, kutokana na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Pillay anasema kuwa Guatemala imeandikisha historia kwa kuwa nchi ya kwanza kumuhukumu kiongozi wa zamani  kwenye mahakama yake binafsi na kuwapongeza wahanga wa uhalifu uliotendeka nchini humo. Ríos Montt alihukumiwa kifungo cha miaka 80 kutokana na mchango wake wakati alipokuwa uongozini kati ya mwaka 1982-83 ambapo watu 1,771 waliuawa na maelfu ya wengine wakalimika kuhama makwao na dhuluma zingine.

Mahakama iligundua kwa uhalifu huo ulitendwa kupitia kwa mipango wa jeshi ukiwalenga wale waliokuwa wakitajwa kuwa maadui. Majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo walifikia uamuzi kuwa Ríos Montt aliamrisha  kufanyika kwa uahalifu huo.