Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza uchaguzi Pakistan

Ban apongeza uchaguzi Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kukamilika kwa amani uchaguzi mkuu wa Pakistan ni ishara kwamba taifa hilo limepiga hatua na kukomaa kidemokrasia .

Ban amepongeza hali iliyoonyeshwa na vyama vya siasa akisema kuwa pande zote zilizingatia uadilifu na kuheshimu misingi ya utunzaji wa amani ya nchi.

Ameeleza kuwa uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa juma, umeweka rekodi ya aiana yake kwa wananchi kubadilishana utawala wa kiraia kwa njia ya amani na utulivu.

Pia alizungumzia kufurahishwa kwake na namna idadi kubwa ya wapiga kura wengi wakiwa vijana walivyojitokeza kushiriki uchaguzi huo ambao umekamilika kwa kiongozi wa zamani Nawaz Sharif kufanya vizuri