Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa misitu na wadudu ni mkubwa kukabili njaa:FAO

Mchango wa misitu na wadudu ni mkubwa kukabili njaa:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema misitu na rasilimali zilizomo vina mchango mkubwa katika kuisaidia dunia kukabiliana na tatizo la njaa. Taarifa zaidi na George Njogopa. (SAUTI YA GEORGE)

Zaidi ya watu bilioni moja duniani kote hutegemea misitu kuendesha maisha yao ya kila siku ikiwemo chakula na uvunaji wa malighafi.Mkurugenzi wa FAO Graziano da Silva amesema kuwa wanyama wa msituni pamoja na viumbe wengine, kutoa mchango mkubwa kuimarisha afya ya binadamu wakati majani ya mimea mingi ikitegemewa pia na mwanadamu huyokamasehemu ya kupatia madini na ukamilishaji wa mlo kamili.

(SAUTI YA GRAZIANO)

Kulingana na utafiti huo mpya wa FAO asilimia kubwa ya lishe ya binadamu inayotoka kwenye misitu inatoa kwa jamii ya wadudu . FAO inasema kuwa kiasi cha watu bilioni 2 hutegemea mlo kamili wa kijadi kutoka kwa jamii ya wadudu.