Viongozi wa Baha’i waachiliwe Iran: UM

13 Mei 2013

Kikundi cha wataalam wa haki za binadamu wameitaka mamlaka ya iran kuwaachilia huru viongozi 7 wa jamii wajulikanao kama Yaran, ikikaribia miaka mitano tangu wakamatwe, kufungwa kwao kukitajwa kama holela na kundi la UM kuhusu kukamatwa kiholela kwa watu mnamo novemba 20 2008

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

Serikali ya Iran inapaswa kuonyesha kujitoa kwake katika kuhakikisha uhuru wa dini na kuwaachilia mara moja wafungwa hawa wa dhamiri amesema mwakilishi maalum wa haki za binadamu Ahmed Shaheed. Kesi hizi zinaonekana kushindwa kulinda viwango vya hukumu ya haki na kuhatarisha uhuru wa dini Iran

Watu hao walikamatwa na kuwekwa vizuizini kwa miezi 20 bila mashataka yeyote na bila nafasi ya kupata mawakili.Baadaye walihukumiwa kifungu cha miaka 20 mnamo Agosti 2010 na mashatak ya upelelezi na kuhatarisha usalama wa nchi na ufisadi.

Katiba ya Iran inatambua na kulinda dini nne ikiwemo Islam, ukristo na uyahudi na Zoastrianism. Bahai’s kwa upande wake haitambuliwa na katiaba.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa masikitiko yake kuhusu sheria kandamizi na sera ambayo inawazuia wafuasi wa Baha’is kuunda vikundi vya dini, kujiunga na vyuo vikuu na kuajiriwa katika sekata ya umma Iran.

Bw. Shaheed amesema anasikitika kwamba baada ya miaka mitanao viongozi hawa wa Yarana wananyimwa haki zao, na Baha’i wa Iran wako hatarini zaidi kuendeleza shughuli katika jamii aidha ameitaka jamii ya kimataifa, wakiwemo viongozi wa kidini kujiunga katika ombi kwa serikali ya Iran kuwachilia viongozi wa Baha’is.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter