Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kuachiliwa kwa walinda amani wa UNDOF

Ban akaribisha kuachiliwa kwa walinda amani wa UNDOF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha kuachiliwa kwa walinda amani wanne wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha uangalizi wa utiaji chini silaha, UNDOF, ambao walikuwa wamezuiliwa tangu Mei 7 karibu na eneo la Al Jamlah nchini Syria.

Bwana Ban ametoa shukrani kwa msaada wa serikali ya Qatar na wengine walohusika katika kuhakikisha walinda amani hao wameachiliwa.

Katibu Mkuu amerejelea wito wake kwa pande zote zinazozozana kuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa hawaegemei upande wowote.

Walinda amani wa UNDOF wanaangalia utekelezaji wa makubaliano ya utiaji chini silaha kati ya Israel na Syria. Bwana Ban ametoa wito kwa pande zote ziheshimu uhuru wa kutembea na usalama wa wafanyakazi wa UNDOF.