Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulizi la bomu kusini mashariki mwa Uturuki

Ban alaani shambulizi la bomu kusini mashariki mwa Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulizi la bomu lilitokelezwa mnamo Jumamosi kwenye mji wa Reyhanli, katika mkoa wa Hatay nchini Uturuki. Kwa mujibu wa ripoti za awali, watu arobaini wameuawa katika shambulizi hilo, na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa.

Bwana Ban amelaani vitendo vyote vya kigaidi, na kusisitiza kuwa hakuna sababu au manung'uniko yoyote yanayoweza kufanya mashambulizi yanayowalenga raia yakubalike.

Katibu Mkuu amesema anatumai kuwa walotekeleza shambulizi hilo watatambulika haraka na kuwajibishwa kisheria, na kutuma risala ya rambirambi kwa waathiriwa na familia zao pamoja na serikali ya Uturuki, na kuwatakia nafuu haraka waliojeruhiwa.