Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvumilivu, ujasiri na kutokata tamaa vilinitia moyo: Balozi Mahiga

Uvumilivu, ujasiri na kutokata tamaa vilinitia moyo: Balozi Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ambaye anamaliza jukumu lake mwezi ujao amesema miaka mitatu ya jukumu hiyo ilikuwa na changamoto nyingi lakini mambo makuu matatu yalimwezesha kusonga mbele na kukamilisha jukumu alililokuwa amepewa. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio hii, Balozi Mahiga amesema kuna wakati alikata tamaa lakini hakurudi nyuma.

(SAUTI MAHIGA)

Basi ili kupata mengi zaidi kuhusu yale aliyokumbana nayo Balozi Mahiga, kile kilichompa moyo na mambo ya kuzingatiwa na wanaoendeleza mchakato wa amani Somalia, tembelea tovuti yetu.