Pillay ataka wale wanaondesha uhalifu nchini Syria kuchukuliwa hatua

10 Mei 2013

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa ripoti kuhusu mauaji ya halaiki nchini Syria yaynayoendeshwa na serikali ya Syria na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali siku za hivi majuzi yataichochea jamii ya kimataifa kuhakikisha wale waliohusika kwenye ukiukaji huo wa haki za binadamu wamewajibika. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Pillay pia ameelezea hofu kutokana na ripoti zinazosema kuwa wanajeshi wamekuwa wakiuzingira mji ulio magharibi mwa Syria wa Qusayr akisema kuwa huenda uhalifu zaidi ukatendeka. Pillay anasema kuwa amesikitishwa na mauaji ya wanawake , watoto na wanaume kwenye kijiji cha al-Bayda na sehemu zingine zikiwemo Baniyas mauaji yaliyoonekana kama kampeni iliyolenga jamii fulani zinazokisiwa kuunga mkono upinzani. Picha za kutisha za mirundikano ya maiti na zingine zilizochomwa zikiwemo za watoto zimeonekana baada ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji kuvamia maneo ya al-Bayda na sehemu za Baniyas wiki iliyopita. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

makubalino kati ya Urusi na Maraekani ya kushirikiana katika kuitisha mkutano wa kimataifa wa kutafuta suluhu la kisiasa kuhusu mzozo ulio nchini Syria.