WHO yapeleka maafisa Saudia kufuatia mlipuko wa coronavirus:

10 Mei 2013

Maafisa wawili wa shirika la afya duniani WHO wamekwenya nchini Saudia Arabia Jumatano wiki hii ili kukutana na maafisa wa wiraza ya afya ya taifa hilo la Kiarabu kutathimini hali ya mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha maradhi ya mfumo wa hewa kwa binadamu.

WHO inasema lengo kubwa la ziara hiyo ni kuelewa hali halisi na kutoa muongozo unaohitajika.Ziara hii ya WHO ni tofauti na ile ya wataalamu wa kisayansi walioalikwa na serikali ya Saudia ingawa maafisa wa WHO huenda wakakutana pia na baadhi ya wanasayansi hao wa kimataifa.

Uchunguzi wa serikali ya Saudia na wanasayansi walioalikwa unaendelea kubaini chanzo cha mlipuko huo na jinsi ya kuudhibiti.

WHO imerejea kusisitiza kwamba hadi sasa hakuna ushahidi wowote wa nini chanzo cha maambukizi hayo kwa binadamu na hakuna ushadi wa kusambaa kwa kiwango kikubwa katika jamii.