Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yalaani uingizaji watoto jeshini CAR

UNICEF yalaani uingizaji watoto jeshini CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limelaani vikali vitendo vinavyoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vya kuwaingiza watoto jeshini na kukatili maisha hayo.

Shirika hilo linasema vitendo hivyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za haki za watoto na haki za binadamu za kuishi kwani watoto wengi wanaposhiriki vitani hupoteza maisha yao na wengine kusalia na vilema vya maisha.

UNICEF imezitolea wito pande zote katika machafuko Jamhuri ya Afrika ya kati kuheshimu sheria za kimataifa na kuzingatia haki za watoto. Pia imezitaka pande hizo kuchukua hatua za haraka kuwalinda watoto walioathirika na vita na kuwaachilia mara moja watoto wote walioingizwa vitani na makundi mbalimbali ya watu wenye silaha. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)