Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asifu mazungumzo kati ya Urusi na Marekani kuhusu Syria

Ban asifu mazungumzo kati ya Urusi na Marekani kuhusu Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekaribisha tangazo kuhusu Syria kutoka kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani seneta John Kerrry. Ban pamoja na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu nchini Syria Lakhdar Brahimi wanasema wanaamini kuwa suluhu la kisiasa ndiyo njia ya pekee ya kumaliza mzozo uliopo. Wanasema kuwa lengo litakuwa ni kumaliza ghasia kufanya mabadiliko na kuafikia Syria iliyo mpya ambapo haki ya jamii zimelindwa na matarajio yote na haki ya wnaanchi wa Syria yametimizwa.