Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheikha Jawaher achaguliwa kuhamasisha kazi za UNHCR

Sheikha Jawaher achaguliwa kuhamasisha kazi za UNHCR

Sharjah's Sheikha Jawaher Bint Mohammed Al Qasimi ametangazwa kuwa ndiye mtu mashuhuri katika Umoja wa falme za kiarabu, katika sherehe maalumu iliyofanyika wiki hii kwenye eneo la Ghuba.

Mumeo Sharjah, mtawala Sheikh Sultan Bin Mohammed Al-Qasimi,na watu wengine wa heshima ni miongoni mwa wageni waliohudhuria sheria hiyo iliyofanyika siku ya jumanne.

Akiwa mtu mashuhuri na muhimu wa eneo hilo, Sheikha Jawaher anatazamia kuchukua jukumu kubwa la kuhamasisha watu kuhusu kuwatambua wakimbizi na nafasi ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR lakini zingatio likiwa ni kwa watoto.

Mwenyewe amepokea wadhifa huo akisema kuwa hiyo ni heshima kubwa kwake.