Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tupanue wigo wa ushirikiano ili kumhakikishia binadamu usalama duniani

Tupanue wigo wa ushirikiano ili kumhakikishia binadamu usalama duniani

Amesema migogoro ya zamani bado inatokota, migogoro mipya inaibuka na kwamba ghasia ni tatizo hata kwenye nchi zisizo na mizozo huku wanawake na wasichana wakiwa hatarini zaidi.

Bwana Ban amesema hayo ni matatizo makubwa yanayotishia usalama wa binadamu lakini akasema kuna dalili za matumaini huku akipongeza mwamko kutoka duniani kote hususan vijana wa kudai haki, utu, na demokrasia ya kweli.

Hata hivyo amesema matukio ya hivi karibuni yamekuwa fundisho na hivyo kuna mambo makuu mawili ya kufanya kwa ajili ya usalama wa binadamu duniani, Mosi..

(SAUTI YA BAN)

"Huwezi kukomesha umaskini bila kuwawezesha wanawake na wasichana . Huwezi kuanzisha amani ya kudumu bila kuheshimu haki za binadamu. Huwezi kufanikiwa kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi bila kubadilisha mifumo ya nishati duniani . Yatupasa kupiga hatua kwa pande zote."

Pili amesema ni wakati wa kuongeza wigo wa ushirikiano na wabia wa jadi kama vile serikali na mashirika ya kiraia, lakini pia wasomi, wafanyabiashara, wasamaria wema na makundi mengine ili kusaidia kutokomeza umaskini na kujenga amani ya kudumu.

Katibu Mkuu amesema wakati huu ambapo dunia inapambana kufanikisha malengo ya milenia na kuandaa mkakati wa maendeleo baada ya mwaka 2015, juhudi hizo lazima zizingatie usalama wa binadamu.