Somalia yafungua ukurasa mpya

8 Mei 2013

Harakati za kuweka amani nchiniSomaliazinaendele kupata matumaini huku serikali ya Somalia kujikwamua kutokana na machafuko yaliyoikumba  kwa muda wa miongo miwili iliyopita.

Somalia imeshudia mabadiliko makubwa kama vile kupata uhuru wa miji kadhaa ikiwemo Mogadishukutoka kundi la waasi la al shabaab. Jambo lililodhahiri ni kwamba ni jukumu la wasomali kulijenga taifa lao, Ungana na Grace Kaneiya kwenye makala ifuatayo.

Mjini Mogadishu, shughuli za usafiri zikiendelea wakati mkutano kuhusu mustakabali wa amani nchini Somaliaukiwa umehitimiswha huko Uingereza, raia wa nchi hiyo wenye jukumu la ujenzi wa taifa lao wameonyeha matumaini makubwa kwamba matokeo ya mkutano huo yatakuza ustawi wa taifa lao.

Ugas Ali-Hashi, miongoni mwa wazee wanaoheshimika katika jamii anasema

(SAUTI)

 "Nina furahi kwamba mkutano wa London unaendelea na tunatarajia matokeo mazuri iwapo dunia itaendelea kubaki kuwa mwaminiifu kwetu."

 Mamia ya Wasomali wanaoishi ughaibuni wamerejea nyumbani Moghadishu na katika miji mingine ili kuchangia katika kufufua uchumi wao. Ha wale wenye ujuzi ambao ndio hasa wanahitajika kama mhandisi Abdullahi Mohamed Abdi wanasema wana imani kuwa mikutanokamahiyo inazidi kufungua mlango.

 Abdillahi:”

(SAUTI)

 “Natumaini kwamba mkutano wa London utasaidia kuimarisha usalama , uchumi, na maisha ya kila siku ya watu wetu.Wasomali wanatakiwa kufanya kazi pamoja kuijenga nchi yetu , hakuna mwingine atakaye fanya hivyo.”

Zaidi ya miongo miwili juhudi zikiwemo za kimataifa zimefanyika kuhakikishaSomalia inapata serikali ya kudimu na kuwa na amani. Lakini Wasomali wanasema kufanyikisha azma hiyo ni jukumu la Wasomali wenyewe. Abdirizak Mohamed Osman ni muuza duka anaeunga mkono kauli hiyo

 Osman:(SAUTI)

 “Mkutano wa London pekee hauwezi kutatua matatizo yetu. Wasomali tunahitaji kushirikiana na kukubaliana njia za kushirikiana madaraka na kumaliza tofauti zetu.”

Wadau na marafiki wa SDomalia kutoka mataifa 50 wameshiriki mkutano huo ukiwemo Umoja wa mataifa na shirika la fedha duniani IMF.