Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu huenda zikasahaulika Misri: Pillay

Haki za binadamu huenda zikasahaulika Misri: Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametaka serikali ya misri  kuchukua hatua kuhakikisha kuwa kipengee cha katiba kuhusu mashirika ya umma kimewekwa wasi ili kuweza kuchunguzwa na wataalamu wa masuala ya haki za binadamu nchini Misri na kutoka nchi za kigeni na kuwekwa kuambatana na viwango vya kimataifa kabla ya kuidhinishwa.

Pillay amesema kuwa itakuwa ni hatari ikiwa katiba mpya inatoa mamlaka kwa mahakama ikiwa majaji watakuwa wakiteuliwa moja kwa moja na rais.

Anasema kuwa ikiwa sheria hiyo itawekwa itakandamiza shughuli za mashirika ya umma na pigo kwa yale yaliyotimizwa kupitia kwa mabadiliko ambayo yameshuhudiwa nchini misri. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

 (SAUTI YA RUPERT)

“Tunaisihi serikali iwe makini kuhakikisha vipengele vinawianga na viwango vya kimataifa. Iwapo wataikosea sheria hiyo, basi itakuwa na madhara makubwa kwa Misri katika kipindi hiki muhimu ambacho mashirika ya kiraia yanaelekea kuwa na dhima muhimu ya ujenzi wa Misri mpya yenye usawa na ya kidemokrasia.”