Brahimi akaribisha tamko la Urusi na Marekani

8 Mei 2013

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa nchi za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Lakhdar Brahimi, ambaye anahudhuria mkutano wa wazee huko Ireland, amekaribisha tamko lililotolewa  Jumanne mjini Moscow na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergey Lavrov na yule wa Marekani John Kerry kuhusu Syria. 

Amesema hii ni habari ya kwanza ya kutia matumaini kuhusu Syria taifa ambalo limeghubikwa na huzuni na machafuko kwa muda mrefu sasa. 

Lakhdar Brahimi mara nyingi amezitaka Marekani na Urusi kutumia uongozi wao kufanya kazi pamoja ili kuanzisha mchakato wa utekelezaji wa azimio la Geneva la Juni 30 mwaka 2012 kuhusu Syria.

Taarifa iliyotolewa Moscowni hatua ya kwanza ya kusonga mbele katika kutatua mzozo wa Syria.

Bwana Brahimi amesema kuna kila sababu ya kutarajia kwamba wajumbe wengine watatu wa kudumu wa baraza la usalama na wajumbe wengine wote wa baraza hilowatashirikiana pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuendeleza mchakato huo. 

Ameongeza kuwa pia ni muhimu kwa ukanda mzima wa Mashariki ya Kati wakaunga mkono mchakato huo wa kuleta amani ya Syria.