Ubunifu wa sekta binafsi unaweza kusaidia kukabiliana na changamoto za sasa: Ban

7 Mei 2013

Umoja wa mataifa utahakikisha ya kwamba unatumia vyema nafasi na ubunifu wowote ule uliopo katika kizazi cha sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon kwenye tukio lililomkutanisha na wakurugenzi wakuu wa mashirika makubwa ya kibinafsi kama Benki ya JPMorgan Chase, na kampuni nyingine za kimataifa kama vile Johnson $ Johnson, na Maerke ambazo hujihusisha na masuala ya afya.

Hafla hiyo inaenda sambamba na kampeni ya “Kila mwanamke, Kila mtoto” kwa lengo la kuona jinsi ubunifu wa sekta ya kibinafsi unavyoweza kuigwa na kutumiwa katika kuyatatua matatizo ya ulimwengu sasa.

Akipigia debe ushirikiano kati ya sekta ya kibinafsi na sekta ya umma, Bwana Ban amesema katika karne ya 21, hakuna taasisi, wala nchi ambayo pekee inaweza kuyatatua matatizo ya ulimwengu na changamoto zilizopo, hata iwe na nguvu na utajiri wa aina gani.