Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika Kaskazini zapatiwa fedha kuendeleza mradi wa nishati ya sola

Nchi za Afrika Kaskazini zapatiwa fedha kuendeleza mradi wa nishati ya sola

Nchi za Afrika Kaskazini zimetengewa kiasi cha dola za Marekani bilioni 7.6 toka kwa fuko  maalumu la ufadhili miradi ya hali ya hewa, ili kuendeleza mradi wa nishati ya umeme wenye ukubwa wa megawatt 1,120.

Mradi huo ambao unategemea kutumia nguvu za sola, unatekelezwa katika nchi sita Algeria, Misri, Jordan,Libya, Morocco na Tunisia.

Rais wa wakala wa sola nchini Morocco Mustapha Bakkoury ameunga mkono kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha akisema kuwa kutatoa msukumo kwa wahisani wengine kujiingiza kwenye mradi huo ili kuufanikisha.

Mradi huo ulikubaliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009 kama sehemu ya kufufua uchumi wa nchi zilizokumbwa na vuguvugu la mapinduzi ya kiarabu na kushuhudiwa tawala kadhaa zikisambaratika.