Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la UM la kuchunguza haki za binadamu DPRK latajwa

Jopo la UM la kuchunguza haki za binadamu DPRK latajwa

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeteua tume ya watu watatu ambayo itachunguza uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Korea Kaskazini. Tume hiyo inataongozwa na mwenyekiti Michael Donald ambaye ni jaji wa zamani wa mahaka kuu nchini Australia akishirikiana na Bi Sonja Biserko wakili wa masuala ya haki za binadamu kutoka Serbia na Marzuki Darusman ambaye ni mjumbe maalum wa masuala ya haki za binadamu nchini Korea Kaskazini. Azimio lililopitishwa na baraza la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwaka huu liliipatia majukumu tume hiyo kuchunguza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Korea Kaskazini.

Tume hiyo itachunguza ukiukaji wa haki za binadmu kuhusu haki ya kupata chakula , hali kwenye magereza , dhuluma na mateso , kuzuiliwa kinyume na sheria , ubaguzi , ukosefu wa uhuru wa kujierleza, haki ya kuishi na kutembea , kutoweka kwa watu na kutekwa nyara kwa raia wa kigeni. Tume hiyo inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake baada ya mwaka mmoja. Rolando Gomez ni msemaji wa tume ya haki za binadamu.

(SAUTI YA ROLANDO GOMEZ)