Raia wengi wa Syria wanaendelea kuhama makwao: OCHA

7 Mei 2013

Watu zaidi wanaendelaea kuhama ndani mwa Syria ambapo kwa kipindi cha miezi kadha iliyopita idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Syria imeongezeka mara dufu kutoka watu milioni 2 hadi watu milioni 4.25. Idadi kubwa ya wakimbizi hao wamekusanyika kweneye mji wa Aleppo na vitongozi vya mji wa Damascus kwa mujibu wa Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA. Hata baada baada ya kuvurugika kwa usalama hatua za utoaji misaada kwa maeneo yaliyoathiriwa zimepigwa.Tarehe 25 mwezi uliopita misaada ilifika maeneo ya Ter Mallan na Al Ghan eneo la Hons ikipeleka chakula na bidhaa zingnie zisizo chakula kwa karibu watu 24,000.

Kwa ujumla kati ya mwezi Januari hadi Aprili watu 764,000 wamefikiwa na misaada inayoongozwa na Umoja wa Mataifa kwenye maeneo yaliyo vigumu kufikiwa. Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LAERKE)