Afya ya watoto na akina mama wazazi ipewe kipaumbele: Ban

6 Mei 2013

Kuwekeza katika afya ya wanawake na watoto huzaa matunda makubwa kwa watu binafsi, familia, jamii, na hata kwa siku zijazo tutakazo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, wakati wa mkutano wa Baraza la masuala ya kiuchumi na kijamii katika Umoja wa Mataifa.

Bwana Ban amesema, katika siku zilizosalia hadi tarehe ya mwisho ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, (MDGs), juhudi zitatakiwa kuwekwa katika maeneo yenye umuhimu zaidi. Amesema kwa sababu hiyo, amefanya kuboresha afya ya akina mama na watoto suala la kipaumbele.

Katibu Mkuu amesema ingawa vifo vya watoto vimepungua kwa takriban nusu na vile vya akina mama katika uzazi kupungua kwa asilimia 40, juhudi zaidi zinatakiwa kufanywa.

(SAUTI YA BAN)

Bwana Ban amekisifu kituo cha kimataifa cha utafiti katika magonjwa ya kuharisha cha Bangladesh kwa kuongoza katika juhudi za kuendeleza afya ya watoto na akina mama wazazi.

\