Baraza la usalama lalaani vikali mauaji ya chifu wa Dinka

6 Mei 2013

Wajumbe wa baraza la usalama leo wamelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya Misseriya dhidi ya msafara wa mpago wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Abyei UNSFA mwishoni mwa wiki.

Mashambulizi hayo yamekatili maisha ya bwana Kuil Deng Kuol ambaye ni alikuwa chifu wa Ngok Dinka na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Ethiopia huku yakijeruhi wengine watatu.

Wajumbe wametuma salamu za rambirambi kwa jamii ya Ngok Dinka, serikali ya Ethiopia na UNSFA.

Wajumbe hao wa baraza wameshukuru kwa ahtua iliyochukuliwa na Rais Salva Kiir, Rais Omar Al-Bashir, viongozi wengine wa serikali hizo mbili na pia Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika kwa kutuliza hali hiyo.

Baraza la usalama limesema litaendelea kusaidia mpango wa UNSFA na kuzitaka pande zoteSudankushirikiana na mpango huo katika kuchunguza matukiokamahayo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter