Guterres amshukuru amiri wa Kuwait kwa kutia shime operesheni za UNHCR Syria

6 Mei 2013

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR António Guterres ametembelea Kuwait na kumshukuru kwa dhati kiongozi wa nchi hiyo Sheikh Sabah Al-Ahmed Al-Jaber Al-Sabah, kwa mchango wake wa dola Milioni Mia Moja na Kumi za kusaidia operesheni za shirika hilo huko Syria kama anavyoripoti George Njogopa.

 (SAUTI YA GEORGE)

Guterres alikutana na mwenyeji wake Mtukufu Sheikh Saba katika jengo la kifalme mwishoni mwa juma,ambako alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za UNHCR kutokana na msaada huo ambao ulitangazwa hivi karibuni mjiniGeneva, Uswisi. 

Kiwango cha fedha kilichoahadiwa kutolewa naKuwait ni sehemu ya msaada unaofikia dola za Marekani milioni 300, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kutolewa na taifa la Kiarabu.

Akizungumzia msaada huo, Guterres alisema kuwa, kiasi cho cha fedha kitarahisisha shughuli za utoaji wa misaada ya dharura kwa mamia ya wakimbizi waSyriaambao wako katika hali mbaya. 

Akiwa nchiniKuwait, Kamishna Guterres pia alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia Waziri wa Mambo ya Nje,Sheikh Sabah Al-Khalid Al-Sabah.