Ban alaani mauaji ya chifu wa jamii ya Ngok Dinka

6 Mei 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani vikali mauji ya chifu wa jamii ya Ngok Dinka , Dengkuol Deng na mlinda amani moja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani eneo la Abyei UNISFA baada ya msafara wao kushambuiliwa hii leo ambapo pia walinda usalama wawili walijeruhiwa vibaya.

Katibu mkuu ametuma rambi rambi zake  kwa jamii ya Ngok Dinka, kwa serikali ya Ethiopia kwa familia za wale waliouawa na kujeruhiwa.

Ban amezitaka  serikali za Sudan Na Sudan Kusini pamoja na jamii za Ngok Dinka na Messeriya kuwa watulivu. Katibu mkuu amesema kuwa kwa mara nyingine hii inaonyesha umuhimu wa mataifa kuweza kubuni taasisi kuambatana na makubaliano ya tarehe 20 mwezi Juni mwaka 2011.