Ni wakati wa kutumia fursa zilizopo Haiti:Sean Penn

6 Mei 2013

Huu ni wakati wa kutumia fursa zilizopo Haiti, taifa ambalo linaweza kuwa na manufaa makubwa kwa mataifa mengine na kwa watu wake hasa kwa kutumia sekta binafsi.

Mtazamo huo umetolewa na Sean Penn mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la msaada kwa Haiti J/P HRO.

Akizungumza kwenye makao makuu ya Bank ya Dunia mjini Washington DC Penn amesisitiza kwamba Haiti imepiga hatua kubwa tangu kutokea kwa tetemko la ardhi mwaka 2010 na ameitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kulisaidia taifa hilo wakati huu likizaliwa upya.

Ameongeza kuwa Wahaiti wengi wako tayari kuwa jeshi la kuleta mabadiliko kinachotakiwa ni kuwabaini na kuwapa muongozo.

Amesema ingawa hakuna njia raihi ya kukabiliana na majanga, cha muhimu ni kwa mashirika kufanya kazi pamoja kwani hakuna suluhu bila ushirikiano.