Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati zinazofuatilia haki za binadamu zijengewe uwezo: Pillay

Kamati zinazofuatilia haki za binadamu zijengewe uwezo: Pillay

Kikao cha tano cha kamati dhidi ya utesaji ya Tume ya haki za binadamu kimeanza huko Geneva, Uswisi ambapo mwenyekti wa Tume hiyo Bi. Navi Pillay amezungumzia umuhimu wa ubora wa ripoti zinazoandaliwa na waatalamu baada ya tathmini wanazofanya na kusema tayari kuna nchi zimeomba msaada wa kujengewa uwezo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(TAARIFA ASSUMPTA)

Kamati dhidi ya utesaji ni moja ya kamati Kumi za Tume ya Haki za binadamu zinazoundwa na wataalamu huru wanaochaguliwa kufuatilia ukiukwaji wa haki mbali mbali za kibinadamu miongoni mwa nchi wanachama wa mikataba ya haki za binadamu.

Akifungua kikao hicho Kamishna Mkuu Navi Pillay amesema nchi za Afrika tayari zimeomba kujengewa uwezo wa stadi za kuandika ripoti hizo ili kuepuka kuacha masuala ya kimsingi katika ripoti zao.

(SAUTI YA PILLAY)

Bi. Pillay ameshukuru mashirika ya Umoja wa Mataifa kama lile la watoto, UNICEF na lile la wanawake UN-WOMEN kwa kuwa bega kwa bega kusaidia kuwajengea uwezo wahusika wanaoandika ripoti za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.