Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga alaani shambulio la bomu na mauaji Mogadishu

Mahiga alaani shambulio la bomu na mauaji Mogadishu

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, amelaani vikali shambulizi la bomu lililotekelezwa mnamo Mai 5 kwenye kituo cha Kilometer 4 mjini Mogadishu, na ambalo liliwaua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine. Duru zinasema shambulizi hilo liliulenga msafara wa wajumbe wa kimataifa.

Katika taarifa yake, Balozi Mahiga amelitaja shambulizi hilo kama kitendo cha uoga na kuongeza kuwa halitadunisha hatua za maendeleo ambazo Somalia imepiga katika miezi kadhaa iliyopita.

Halikadhalika amesema mashambulizi dhidi ya raia daima hayawezi kukubalika, na kutoa wito kwa wahusika wote kuachana na vitendo vya ghasia na kuchangia amani na usalama.

Balozi Mahiga ametuma risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wahanga wa shambulizi hilo, na kuwatakia nafuu walojeruhiwa.